MAANDIKO yanasema ‘usitamani mali ya mtu mwigine’!
BWANA Anton John Akiwa ndani ya PINGU
Ni kweli kabisa, onyo hilo lilichukua fursa yake kufuatia njemba mmoja aliyejulikana kwa jina la Anton John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina moja la Chalz.
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo) iliyopo Buguruni- Malapa jijini Dar es Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje alikuwa akiifahamu vyema familia ya Chalz sambamba na mke wake (jina lipo) lakini hilo hakulijali na kumtokia mke wa Chalz ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni shemejiye.
Mitungi na MAKULAKULA YA KUONGEZA STAMINA
JAMAA Anton John Akiwa na mzigo wa besti ake.