MUHINDI KOKO AMBAMBWA NA MKE WA RAFIKI YAKE. YALIYO MKUTA HATOKUJA SAHAU!!!

Yamemkuta! Jamaa mwenye asili ya udosini almaarufu kwa jina la Sharukani wa Vingunguti au wa Dar, mkazi wa Airport jijini Dar, anadaiwa kunaswa laivu ‘akimtumbua’ mke wa rafiki yake, naye ‘kutumbuliwa’ kwa kupewa mkong’oto hivyo kukiri ‘kweli mke wa mtu ni sumu’.






 Ilisemekana kwamba, mumewe huyo alimruhusu kwa kuwa ni utaratibu wa mkewe wa kila mwaka kwenda kuwatembelea wazazi.
 
Ilidaiwa kwamba, kumbe Love hakusafiri kama alivyomuaga mumewe badala yake alimzunguka kwa kutembea na rafiki yake ambapo mashemeji zake walimuona akijiachia viunga mbalimbali vya jijini Dar na Sharukani kama mke na mume bila aibu ndipo wakamtonya J4 na kuwawekea mtego ambao ulipofyatuka, ukawanasa gesti maeneo ya Ilala.

…..Akiminyiwa kichapo.
Muda mfupi baada ya kujiri kwa tukio hilo, wanahabari wetu walipokea taarifa ya kuwepo kwa fumanizi hilo na kufika eneo la tukio ambapo kutokana na foleni zilizosababishwa na shamrashamra za mkesha wa mwaka mpya, walishindwa kuwahi wakati muafaka na kukuta polisi wameshawachukua wahusika.
Hata hivyo, waandishi hao walifanya jitihada za kuzungumza na Jumanne ambaye alifunguka kuwa kwa muda mrefu alikuwa akimuamini mkewe na kamwe hakuhisi uhusiano wao na rafiki yake kwa kuwa aliwahi kumtambulisha mara moja.
“Nina hasira sana, nimemtua lakini ningeweza kumuua kabisa maana kila nikijiuliza ilikuwaje wakaamua kunifanyia kitu kama hicho kwa kweli sipati picha,” alisema J4 akiwa ha hasira na kuongeza:


Akiomba kuachiwa.
“Nimeamua kumrudisha Love kwao lakini nilifuatilia pale polisi kuhusu huyo Sharukani naye sijui alipo maana nilisikia ameachiwa na namba yake hapokei.”
Gazeti hili lilipomtafuta Love kisha kumsomea mashtaka yake alikata simu na hata alipopigiwa tena na kutumiwa ujumbe mfupi hakujibu.
Kwa upande wake Sharukani alikuwa na haya ya kusema: “Mimi ndiye nilianza kuwa na Love kitambo lakini nikiongea nitaonekana mbaya.
“Ni kweli nina mke na familia kwa hiyo tukio hilo ni aibu sana na sijui kama mkinitoa gazetini itakuwaje.”
Source;Global
© Copyright Mombasa Ni Raha Published.. Blogger Templates
Back To Top